Serikali imesema itaendelea
kutoa elimu kwa kushirikiana na taasisi za sekta nyingine ikiwemo viongozi wa
dini katika kuhakikisha mauaji na ukatwaji wa viungo vya Albino vinatokomezwa
nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Mh Kebwe
Stephen Kebwe katika Mkutano wa 20 na wa
Mwisho wa Bunge la 10 la Tanzaniabungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu
swali la msingi la Mh.Matha Umbula aliyetaka kufahamu jitihada zinazofanywa na
serikali kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu.
Mh. Kebwe amesema ugonjwa wa Albinism ni ugonjwa ambao binadamu anazaliwa nao
hivyo ni vyema jamii ikawachukulia walemavu hao kama binadamu wengine kwa
kuwathamini kuwajali na kuwalinda ili
kuweka uwiano uliosawa ili nao wasijihisi kuwa tofauti na wengine hali
inayoweka taswira kama ya kumnyanyapaliwa.
Hata hivyo wakati akiuliza swali la nyongeza Mh. Umbula amesema jitihada za
sasa zinazofanywa na serikali hazitoshi huku akishauri jitihada zilizofanywa
katika kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi zifanyike kupambana na mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) ambayo yamekuwa yakiogofya siku za hivi
karibuni nchini na hata kuhusishwa na imani mbali mbali potofu.
Aidha akiwasilisha bungeni mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio
ya matumizi ya fedha ya ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha
2015/20h16 waziri mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika hotuba yake
ameitaka jamii kuondokana na dhana potofu ya kuamini kuwa viungo vya albino
vinasababisha mtu kuwa tajiri na badala
yake amewataka watanzania kufanyakazi kwa bidii ili kuliongezea pato taifa.
0 comments:
Post a Comment