Image
Image

News Alert:Kukosekana kwa nidhamu ya matumizi ya fedha kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kumechangia bajeti iliyopita kuto fikiwa Lengo.


Kukosekana kwa nidhamu ya matumizi ya fedha kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa na Bunge na kutofuata mpango wa bajeti pamoja na kutokutambua vipaumbekle vya taifa ,kumechangia  kwa kiasi kikubwa malengo yaliyokusudiwa ya bajeti iliyopita kuto fikiwa.
Hayo yamebainishwa Mjini Dodoma  na   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ,  HAMISI KIGWANGALLA wakati akiwasilisha taarifa ya kamati .
Amesema mtiririko finyu wa kutekeleza miradi ya maendeleo ,  hasa katika halma shauri haion eshi nia ya dhati ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha katika taarifa ya kamati hiyo imeishauri serikali kufikiria upya muundo wa Serikali ikiwezekana baadhi ya wizara zipunguzwe ili kuipunguzia mzigo Serikali na kwamba hakuna haja ya kupeleka madar a ka mikoani na h apo hapo kubakisha utitiri wa  wizara.
Kwa upande wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa kambi  ya upinzani kuhusu makadirio ya matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu ,DAVID SILINDE imeitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu fedha zinazotolewa wakati hazikuwepo katika mipango ya halmashauri  ambazo taarifa imedai kuwa zimekuwa zikitumika vibaya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment