Mashahidi wanasema Polisi wawili
walifyatua risasi hewani katika kitongoji cha Butarere ambapo mmoja wao mwanake
alikamatwa na waandamanaji na kumpiga kabla ya kumuachia.
Mwandamanaji mmoja aliwaambia
waandishi wa habari kwamba mwanamke mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi wakati
bomu la mkono lilirushwa katika kitongoji kingine cha mji huo na kuua watu
wawili.
Ikiwa vifo hivyo vitathibitishwa
idadi ya watu waliouawa katika maandamano yaliyoanza tarehe 26 ya mwezi
uliopita kupinga Bwana NKURUNZIZA kugombea muhula wa tatu itakuwa imefikia watu
22.
0 comments:
Post a Comment