Kuna hofu idadi ya watu waliokufa
kutokana na tetemeko hilo la jana huenda ikaongezeka huku msako ukiwa
unaendelea wa helikopta ya msaada ya Marekani iliyopotea ikiwa na watu wanane.
Tetemeko hilo limetokea mji wa
Chautara, kilomita 83 Mashariki ya mji
mkuu wa nchi hiyo, Kathmandu wiki mbili baada ya zaidi ya watu Elfu- 8
kuuawa na tetemeko lililoleta uharibifu mkubwa kwa nchi hiyo.
Maelfu ya watu wa Nepal wamekesha
nje usiku wa kuamkia leo na wengi hawajarejea kwenye nyumba zao kufuatia
tetemeko hilo lililokumba pia maeneo ya kaskazini mwa India, Tibet na
Bangladesh.
0 comments:
Post a Comment