Dismas Lyassa wa pili kutoka
kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM kata ya
Mbingu, wilayani Kilombero.
Dismas akiteta na jambo na
mkewe Rightness, nyuma ni mtoto wao Grace picha na mpiga picha wetu.
Ndugu Wanahabari
Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.
Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.
Nimekuwa nikitembelea vijiji
na kata mbalimbali za Wilaya ya Kilombero. Hivi karibuni nilitembelea kata zote
za wilaya, nilizungumza na wananchi, wengi wao walinishauri kugombea Ubunge.
Wananchi wanaamini kuwa kwa pamoja tutaweza kuendeleza vema gurudumu la
maendeleo kwa kasi zaidi.
Wananifahamu kama mtoto wa
masikini mwenzao niliyewahi kuzunguka mitaani kupiga picha ili kuendesha
maisha, mtoto wa masikini niliyewahi kuwa na ofisi ya kusafisha viatu vya watu
eneo la Ubungo Maziwa kwa mzee Mrisho ili niweze kupata nauli ya kwenda shule
wakati huo nasoma Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Maisha nayafahamu vizuri na
nina uchungu nayo, natamani kushirikiana na wananchi ili kuepukana na maisha
duni. Katika maisha yangu kutokula au wakati fulani kutembea kwa miguu kwenda
chuo CBE na kurudi nyumbani Ubungo Maziwa (nilikuwa naishi kwa dada), lilikuwa
ni jambo la kawaida, kwani maisha yalikuwa magumu mno.
Sauti ya wananchi wa
Kilombero
Kilio cha wananchi pamoja na
mambo mengine ni kwamba wanahitaji kiongozi kijana mwenye nguvu za kuongoza,
kiongozi mwenye ujuzi wa namna ya kuongoza na kutawala, kiongozi ambaye atakuwa
bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi.
Kiongozi ambaye anajua namna ya kuongoza, siyo namna ya kuhonga au kuwalisha
yamini wapiga kura, kwani wanachohitaji watu wa Kilombero ni maendeleo, siyo
zaidi.
Hawahitaji kiongozi ambaye ni
maarufu kwa kutembelea magari ya kifahari, wanahitaji huduma za kijamii kama
shule, hospitali na wao wenyewe kusaidiwa namna ya kubuni miradi ya maendeleo.
Elimu yangu ya juu ni
Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala (Postgraduate Diploma in
Leadership and Governance), kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma-Dar es Salaam
niliyohitimu Aprili 22, 2014. Hata hivyo nje ya elimu nimekuwa nikishughulika
na masuala ya kijamii kupitia kufanya mikutano ya ana kwa ana na jamii katika
masuala ya ujasiriamali, uchumba/ndoa na kadhalika.
Mojawapo sababu za wananchi
kuamini kwamba ninaweza kushirikiana nao kwa ufanisi ni rekodi ambazo wananchi
wenyewe wanazo juu yangu, kwani nimekuwa nao karibu katika mambo mengi ya maendeleo
ikiwamo kushirikiana nao moja kwa moja au vikundi vyao hasa vya
walemavu, kina mama, vijana na kadhalika kama mshauri wao katika suala zima la
namna ya kuviendesha na kuwaunganisha na taasisi au watu wa kusaidiana nao.
Kwa hivi sasa maeneo kadhaa ya
Kilombero yanasaidiwa na mashirika mbalimbali yakiwamo ya nje, baadhi yake ni
kutokana na jitihada zangu….nje ya uandishi wa habari, pia nimekuwa nikimiliki
kampuni ya kuwaunganisha watu na vyuo vya nje ya Global Source Watch (GSW),
ambayo imekuwa ikinipa fursa ya kujuana na watu wengi wa nje.
Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni
raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na
ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha
Mofu, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Juni 26, 1976. Nimewahi kufanya kazi
katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi ikiwamo the Guardian
Limited kama mwandishi wa kujitegemea, Uwazi kama Mhariri, Leo ni Leo kama
Mhariri wa Makala, Mwananchi kama Mwandishi wa makala baadaye mhariri wa jarida
la ndani ya biashara, the Media Project (Marekani) kama mchangiaji nk.
Kwa sasa ni Kiongozi wa
Utafiti hapa nchini (National Lead Researcher) wa taasisi ya kimataifa iitwayo
Global Integrity yenye makazi yake Marekani, pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti
la Mwanahabari, lakini maamuzi haya ya kugombea ubunge ni yangu binafsi hayana
uhusiano wala hayataingiliana na sehemu yoyote ninayofanyia kazi.
Nimewahi kutembea katika nchi
mbalimbali kwa lengo la kwa kusoma na kutembea, baadhi yake ni Marekani, Kenya,
Uganda, Dubai, Thailand, India.
OMBI KWA WASAMARIA WEMA
Napenda kuchukua fursa hii
pia kuwaomba wasamaria wema kuangalia namna ya kusaidiana na wananchi wa
Kilombero kwani wakati huu njia nyingi hazipitiki kwa sababu barabara zimejaa
maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Magari yamekuwa hayapitiki katika
maeneo mengi ya Kilombero kwa sasa.
Kwa mfano sehemu kubwa ya barabara
ya kutoka Ifakara kwenda Mofu haipitiki, kiasi kwamba wagonjwa
wamekuwa hawawezi kubebwa kupelekwa Ifakara ambako ndiko pekee kuna hospitali
ya Wilaya, St Francis. Wapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakibebwa kwa kutumia
baiskeli na hata pikipiki, jambo ambalo limekuwa gumu hasa kwa wajawazito.
Magari ya abiriia hasa Noah
zilizokuwa zikifanya safari kutoka na kuingia Ifakara kutoka vijiji mbalimbali
vya Wilaya ya Kilombero yamesitisha safari kutokana na barabara kujaa maji.
Yapo magari machache hasa ya mizigo ambayo nayo yanafika baadhi ya vijijini kwa
shida yakiwa yamebeba mizigo na abiria hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi
Mvua zimeathiri pia kilimo,
kwani mashamba mengi yamefurika maji, huku kukiwa na njaa kwa baadhi ya
wanavijiji. Hivyo nachukua fursa hii kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka
kusaidia wananchi wakiwamo wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mlimba, Chisano,
Chita, Mkula, Sanje, Uchindile na Utengule
Imetolewa leo tarehe 12, Mei
2015,
na Dismas
Lyassa
(Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM)
0754 49 8972/0712183282
(Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM)
0754 49 8972/0712183282
0 comments:
Post a Comment