Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna
wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi
inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza.
Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015
…...Mwisho……
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015
0 comments:
Post a Comment