Tetemeko la sasa lenye nguvu ya 7.4
ikilinganishwa na la kwanza lililokuwa na nguvu ya 7.8 kwenye kipimo cha
matetemeko cha Richta, limetokea karibu
na mji wa Namche Bazar karibu na Mlima
Everest.
Mtikisiko wake ulifika hadi New Delhi, mji mkuu wa India pamoja na Dhaka,
mji mkuu wa Bangladesh,huku mitikisiko mikubwa ikitokea mji mkuu wa nchi hiyo,
Kathmandu ulioharibiuwa vibaya na tetemeko la mwezi uliopita.
Taarifa zinasema wakati wa tetemeko hilo
lililodumu kwa sekunde 30 , watu
walikimbia kutoka nje ya nyumba zao na majengo mengine,na taarifa za awali
zinasema watu wane wamekufa.
0 comments:
Post a Comment