Image
Image

News Alert:Maziwa yasiyo faa kwa matumizi ya binadamu yakamatwa na TFDA*Yadaiwa yanasababisha madhara kwa kuzaliwa watoto wenye vichwa vikubwa.


Mamlaka ya chakula na dawa nchini Tanzania TFDA imekamata vipodozi katoni 45  pamoja na maziwa yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu Box20 vililvyokuwa vikisafirishwa kinyume na sheria katika basi la Taqwa kutoka kampala nchini uganda kwenda jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukagua basi hilo mkaguzi wa TFDA kanda ya mashariki Dokta. Ediga Mahundi amesema  walipata tarifa za siri kutoka kwa wasamaria wema  ambapo waliweka mtego katika mzani wa Kihonda mjini morogoro na kufanikiwa kukamata vipodozi hivyo.

Ameeleza  kuwa  vipodozi hivyo havifai kwa matumizi ya binadamu na vimekuwa vikisababisha tatizo la watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa na hivyo kuwa na madhara.

Kwenye hali ya kushangaza  abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi hilo wameonekana kunywa  maziwa yaliyokamatwa na mamlaka ya chakula  na dawa wakidai maziwa hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Hata hivyo wamezitaka mamlaka husika kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri kabla ya kuondoka na kuigia nchini ili kubaini wale wote wanasafirisha bidhaa zisizo na ubora.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment