Waandamanaji
watatu wameuawa wakati polisi walipokuwa wakiwatawafanya waandamanaji
katika mji wa Bujumbura nchini Burundi
ambao walikuwa wakipinga kitendo cha Rais Piere Nkurunzinza kugombea kiti cha
urais kwa awamu ya tatu.
Waandamanaji
hao waliuawa baada ya jitihada za polisi wa nchini hiyo kuwataka
watawanyike kawa amani kushindikana na pia kitendo cha polisi kufyatua risasi
za moto hewani kuonekana kudharauliwa na wananchi hao na kisha polisi kuamua
kuwafyatulia waandamanaji.
Kwingineko nchini huko baadhi ya watu ambao
wamekamatwa na polisi kutokana na maandamano hayo imebainika kuwa ni watoto
wadogo ambao walishiriki katika maandamano kuwaunga mkono wazazi pamoja na
walezi wao kupinga kitendo cha rais Nkurunzinza kugombea kwa awamu ya tatu.
Inakaridiwa kuwa zaidi ya raia wa burundi laki moja na ishirini wapo
katika makambi ya wakimbizi katika nchi za Tanzania na Burundi ambapo
wamekimbia vurugu baada ya chama cha CNDD -FDD kumpitisha rais
Nkurunzinza kugombea kiti hicho kwa
awamu ya tatu kinyume na katiba inayomruhusu mtu kukaa madarakani kwa vipindi
viwili tu.


0 comments:
Post a Comment