Waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia
Profesa makame mbarawa amesema sheria iliyosainiwa na Rais ya makosa ya mtandao
itaanza kutumika hivi karibuni baada ya elimu kutolewa kwa wananchi huku akitoa
wito kwa wananchi na taasisi kupeleka maoni yao kwa ajili ya kuifanyia
marekebisho.
Akizungumza jijini Dar es salaam Prof Mbarawa
amesema sheria hiyo tayari imesainiwa na rais baada ya kupitia hatua zote za
kuiboresha ambapo hatua ya mwisho ilikuwa ni ile ya marekebisho yalifanywa na
bunge ambapo baadhi vifungu vilivyolalamikiwa viliboreshwa.
Aidha Prof Mbarawa amesema lengo la sheria
hiyo ni kwa ajili ya kupambana na ongezeko la wizi kuptia mindao, ugaidi
unaofanywa kupitia mitandao,mmomonyoko wa maadili pamoja na uharibifu wa
miundombinu hasa tatizo la ukatwaji wa mkongo wa taifa matukio ambayo amedai
kuwa yamekuwa yakisababisha athari kwa jamii na kwa serikali.
0 comments:
Post a Comment