Serikali imeshauriwa kuunganisha wizara
zinazoshughulikia sekta ya elimu nchini ili kuondoa ama kupunguza uwepo wa
mianya ya matumizi mabaya ya fedha,kuongeza uwazi katika sekta ya elimu pamoja
jambo likalosaidia kupunguza matumizi makubwa ya fedha katika sekta hiyo na
kuwa na bajei inayotekelezeka.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam katika
mjadala uliowashirikisha wadau wa sekta ya elimu na afya nchini ambapo afisa
utafiti na uchambuzi kutoka haki elimu Bwana Makumba Mwemezi amesema licha ya
serikali kutenga kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya elimu katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita ambapo kwa mwaka huu zaidi ya Trilioni tatu nukta
mbili zinatumika katika matumizi ya kawaida badala ya kuelekezwa katika
uwekezaji wa elimu.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa shirika
la afya Duniani WHO Dr.Rufaro Chatora amesema ni muhimu uchambuzi ukafanyika
ili kujua bajeti iliyotengwa pamoja na kuanisha matumizi yake ili kuleta ufanisi
huku Bwana Robert Kasenene ambaye ni mwakilishi wa taasisi ya umoja wa mataifa
hapa nchini akielezea kiwango kidogo cha fedha kilichotengwa na kuelekezwa katika
sekta ya afya hususani katika suala la uzazi wa mpango.
0 comments:
Post a Comment