Saa chache kabla ya kufanyika kwa hafla ya
kumuapisha Jenerali bBuhari kuongoza taifa hilo la nigeria yalifanyika
makabidhiano ya kuongoza taifa hilo kati ya rais aliyeshindwa katika uchaguzi
mkuu uliofanyika mwezi March Bw.Goodluck
Jonathan na rais huyo mteule.
Katika mkesha wa kusubiri kuapishwa kwake
huku burudani zikitawala katika viunga mbali mbali vya nchi hiyo huku wananchi
wa Nigeria wakielezea kuwa wanamatumaini makubwa kuwa kiongozi huyo mpya kuwa
atamaliza mataifa yanayolibili taifa hilo.
Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini
Nigeria wamesema kuwa rais Buhari anakabiliwa na jukumu kuu la kuhakikisha anatokomeza
kikundi cha kigaidi cha kiislamu cha Boko haramu sambamba na kuwaokoa mateka
mbalimbali wanaoshikiliwa na kikundi hicho.
0 comments:
Post a Comment