Agizo hilo la serikali
limetolewa na naibu waziri wa nishati na madini anayeshughulika sekta ya
madini Mh.Charles Kitwanga,baada ya kutembele baadhi ya vijiji na
kushuhudia maefu ya nyumba maarufu kama tegesha ambazo zimejengwa ndani
ya miezi mitatu tu baada ya zaoezi la tathimini kukamilika kwa lengo la
kutaka kulipwa fidia kubwa,ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi
le ambao tayari wamefanyiwa tathimini kupokea fidia yao na kupisha katika
maeneo hayo.
Akito maelezo kwa naibu
waziri huyo wa nishati na madini,meneja uendelezaji wa mgodi wa North
Mara Bw. Abel Yiga,amesema awali walikusudia kuufunga mgodi huo kutokana
na changamoto hiyo ya uvamizi wa maeneo hayo baada ya tathimini ya mwaka
2011 kuonyesha kuwa kiasi cha shilingi bilioni tano kilitajika kulipwa
kama fidia lakini baada ya ujenzi huo kufanywa kinyume na taratibu inahitaji
kiasi cha shilingi bilioni 40 ili kulipa fidia hiyo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi
na viongozi wa vijiji hivyo,wamekiri kuwa tatizo la umasikini ni moja ya
sababu ambayo iliwafanya kujenga majengo hayo lengo la kushawishi kulipwa fidia
kubwa hivyo wameiomba serikali na uongozi wa mgodi kukubali kutoa fidia
kwa wananchi wanaomiliki maeneo hayo kabla ya kufanyika zoezi la
tathimini ya mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment