Kiondo
Mshana Pichani hapo -Mkurugenzi Mtendaji Super Brain Media.
Ijue Kampuni ya Super Brains Media.
Kampuni ya Super Brains
Media Limited ilianzishwa Januari 31,2011 kama Limited,ambayo iko Tegeta jijini
Dar es Salaam,Tanzania ikiwa imesajiliwa kwa namba 81238 na kupewa TIN namba
111898642.
Baadhi ya malengo yaliyo
sababisha kampuni hii kuanzishwa ni haya yafuatayo.
·
Kuanzisha na
kuendesha vyuo vya habari vyenye ubora mkubwa vinavyofundisha Uandishi wa
Habari kwa vitendo hadi ngazi ya chuo kikuu.
·
Kufanya biashara
ya kuchapisha Magazeti,Kutoa ushauri wa kitaalamu na kuendesha
Semina,Washa,Kongamano,Kozi fupi,Kozi ndefu na kutoa elimu kwa wanafunzi wa
vyuo hivyo.
·
Kuandika,kuhariri
na kuchapisha magazeti,majarida,vitabu,daftari pamoja na kufanya kazi za
utafiti.
·
Aidha kampuni hii
ilianzishwa baada ya kufanya utafiti na kubaini kuwa elimu inayotolewa kwa
wanahabari hapa nchini,ina pengo kubwa katika ufundishaji wa masomo ya uandishi
wa habari,ambalo lilihitaji kuzibwa.
1. Mapengo yaliyoonekana ni kwamba:
Vyuo vingi vya Habari nchini vimekosa
elimu ya vitendo katika masomo yanayo tolewa ambayo ndiyo muhimu kwa vijana
chipukizi katika tasnia ya habari nchini.
2. Utafiti uliofanywa na kampuni hii umegundua kuwa elimu
inayotolewa na vyuo vya kawaida pamoja na vyuo vikuu nchini ina utamaduni wa nchi za magharibi.
§ Kwa mfano,walimu asilimia kubwa wanaofundisha vyuo
hivyo wana elimu ya kimagharibi,Vitabu walivyosoma ni vya magharibi kwa hiyo
hata dhana wanayo irithisha kwa wanafunzi ni ya kimagharibi ambayo haifanani
wala hai saidii katika mazingira ya kiafrika.
·
3.Vijana wanao
maliza vyuo na kuajiriwa moja kwa moja katika vyumba vya habari wanashindwa kuiweka
nadharia waliofundishwa katika vitendo kutokana na ukweli kwamba siku hizi
wahariri hawana muda wa kuwaelekeza kuhusu utendaji wa kazi zao katika vyumba
vya habari au kuwapa mafunzo kazini kama ilivyokuwa zamani.
·
Kutokana na
matatizo haya ya kukosa maelekezo,vijana wengi wapya wenye uwezo wanapoajiriwa
husindwa kuakabili mazingira ya vyumba vya habari,hatimaye huchanganyikiwa na
kukimbia taaluma ya uandishi wa habari.
·
Ili kuziba pengo
hili kampuni ya Super Brains Media LTD (SBM), kwa kuanzia imeanzisha chuo cha
Uandishi wa habari kwa vitendo kijulikanacho kama Practical School of
Journalism(PSJ) ambacho kimeshasajiliwa na serikali.
·
Pia kampuni imeanzisha gazeti la uchunguzi
lijulikanalo kama Wajibika ambalo tayari limeshasajiliwa na serikali na
linapatikana mikoa yote nchini Tanzania.
·
Hata hivyo ili
kukamilisha mafunzo ya habari kwa vitendo,kampuni imejitahidi kuwa na studio za
radio na Television ambazo kwa sasa zinapatikana Online kwa majina ya SBM Radio
na SBM Tv,pamoja na Blog.
·
Kwa wale wote
watakao taka kutembelea Blog yetu,inaitwa SBM Broadcast na kuipata kwake
unatakiwa uandike www.sbm broadcast.blogsport.com
ambayo hadi sasa ina jumla ya watu 32,879.->>http://sbmbroadcast.blogspot.com
·
Kutokana na wingi
huu wa watu wanao tembelea Blog yetu. Super Brains Media inawakaribisha wote
kutangaza biashara na matukio mbali mbali katika sbm broadcast pamoja na gazeti
la Wajibika.
¨ Kiondo Mshana.
¨ Mkurugenzi Mtendaji.
¨ Super Brain Media.
Simu:
+255715333186
Au +22767333186
Ofisini:+255 737 227 610
Baruapepe:superbrains2014@gmail.com
0 comments:
Post a Comment