Wakimbizi 31 kutoka Burundi wameripotiwa
kufariki Dunia kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu ulioibuka wiki mbili
zilizopita katika kituo cha mapokezi katika Kijiji cha Kagunga Wilayani Kigoma.
Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu katika
wilaya ya Kasulu mkoani humo, SOSPETER BOYO akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, amesema vifo hivyo vimetokea katika kijiji cha Kagunga na katika
kambi ya wakimbizi ambako walifikishwa wakiwa tayari na maambukizi.
Amesema licha ya kwamba hivi sasa kuna
wagonjwa 46 wanaoendelea na tiba, lakini wamefanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo
kutokana na kuimarisha huduma za afya kwa kushirikiana na mashirika yanayotoa
huduma kwa wakimbizi.
Kwa upande wake , Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, MATHIAS CHIKAWE amesema inafanya jitihada kuhakikisha wakimbzi ambao
kwa sasa wanaishi katika kambi ya wakimbizu wenzao kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo wanapatiwa eneo lao
ili kuepusha msongamano ambao unaweza kuchangia mlipuko wa magonjwa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment