Watu wawili wamefariki dunia na wengine 11
kujeruhiwa vibaya baada ya basi dogo walilokuwa wakitumia
kusafirisha maiti kugongana na basi kubwa la abiria katika eneo la Kihonda
mizani katika barabara kuu ya Morogoro- Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ,Leonard
Paul amesema ajali hiyo imetokea Mei 6 mwaka huu majira ya
saa 9.15, usiku,katika eneo la Kihonda manispaa ya Morogoro,ambapo basi
la kampuni ya Mvula lililokuwa likitokea mkoani Kigoma kwenda
jijini Dar es salaam likiendeshwa na Ramadhan Bakari kugongana na basi
dogo aina ya Toyota Costa likiendeshwa na Hassan Akilima ambayo ilikuwa
imebeba mwili wa marehemu aliyefia nchini China na wanafamilia wakielekea
mkoani Kagera.
Amewataja waliokufa katika ajali
hiyo kuwa ni Othuman Dabaga (43) mkazi wa mwananyama jijini Dar es
salaam na Hamida Said (43) mkazi wa Dar es-salaam.
Aidha waliojeruhiwa katika ajali hiyo
wametambuliwa kuwa ni Hassan Akilimali ambaye ni dereva wa basi
dogo, Lulu Simon,Ruth Antony,Kulwa Mponda,Abdi Mariki,Johari John,Haiba
Suleiman,Tatu hamis,Sophia Suleiman,watoto Aisha Hamis mwenye umri wa miaka
minne na Abdumury Suleiman wa miaka mitatu,wote wakazi wa jijini Dar es
salaam.
Kamanda Paulo amesema polisi wanamshikilia
Dereva wa basi la Mvula,Ramadhan Bakar kwa kusababisha
ajali hiyo na kwamba anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya
upelelezi kukakamilika
Taaarifa zilizotolewa na abiria
waliokuwa walionusurika na waliokuwa kwenye gari ndogo
iliyokuwa ikisafirisha maiti wamedai changamoto ya safari ilianza baada ya kifo
cha ndugu yao,pale familia ya marehemu na mke wa marehemu
walipokuwa kwenye ubishani wa wapi marehemu azikwe,hali iliyowafanya upande
mmoja kukimbilia mahakamani na kufungua shauri lililodumu takribani wiki moja
kabla ya maamuzi.
0 comments:
Post a Comment