Image
Image

Ucheleweshwaji wa ujenzi Hosipitali ya Wilaya ya Longido ni sababu inayochangia wananchi wa kipato cha chini kupoteza maisha.


Kuchelewa kwa ujenzi  wa Hosipitali  ya Wilaya ya Longido Mkoani  Arusha   kumesababisha  asilimia  kubwa  ya  wananchi  wa kipato  cha  chini kupoteza  maisha  na wengine  kuendelea  kutumia  tiba za  jadi, kutibu  magonjwa  yanayohitaji  madaktari  bingwa  kutokana  na kushindwa  kumudu  gharama za  kuwafikisha  katika  hosipitali  za wilaya  za jirani  na ya Mkoa wa Arusha ya Mount  Meru.
Wakizungumza na viongozi  wa Jumuiya  ya Wazazi  Mkoa   wa Arusha  waliotembelea  wilaya hiyo, wananchi hao na baadhi  ya watendaji wa  sekta  ya  afya wamesema,  licha ya kupewa ahadi za ufumbuzi  wa matatizo  yao  hakuna  utekelezaji na wameilaumu  jumuiya  hiyo  kwa kushindwa  kusimamia  maadili ya viongozi  na watendaji  ambao  asilimia  kubwa  hawatimizi  wajibu  wao.

Wakizungumza  baada  ya  kutembelea  Kituo cha  Afya  cha Longido na  kujionea  hali halisi,  baadhi  ya  viongozi  wa jumuiya  hiyo wamewaomba  wananchi  kuendelea  kutoa  ushirikiano  wa  kuwadhibiti  viongozi  na  watendaji wasiofuata  maadili,   kwani  ndiyo njia  pekee  ya kukomesha   tatizo hilo na  inawezekana.

Wilaya  ya Longido  ilianzishwa mwaka  2007,  baada kugawanywa Wilaya  ya Monduli,   lengo  likiwa  ni  kusogeza huduma muhimu  ikiwemo ya  afya  karibu  na  wananchi,  lengo  ambalo  kwa  asilimia  kubwa  bado  halijafikiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment