Rais wa shirikisho la soka barani ulaya Michel
Platini amewambia waandishi wa habari kuwa Blatter amekataa wito wa kujiuzulu.
Platini amesema kuwa kufuatia uamuzi huo UEFA sasa
itashiriki uchaguzi hapo kesho na imewashauri washirika wake kumpigia kura
mpinzani wa Blatter mwanamfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Bara la Afrika limeahidi kumpigia kura Blatter sawa
na shirikisho la bara Asia.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 anawania nafasi ya
kuwa rais wa FIFA kwa kipindi cha tano mfululizo.
Viongozi kadhaa walikuwa wamependekeza kuhairishwa
kwa uchaguzi huo huku wengine wakimtaka ajiuzulu ilikuwepo na mwanzo mpya
katika FIFA.
Awali ,Blatter aliongoza kikao cha dharura cha
wanakamati wakuu wa shirikisho hilo huko Zurich Uswisi.
Kikao hicho kinafuatia hatua ya kukamatwa kwa
maafisa 7 wakuu na polisi huko Zurich Uswisi kwa tuhuma za ufisadi.
0 comments:
Post a Comment