Image
Image

Serikali ya Burundi yapinga shinikizo la kimataifa kuhusu rais wa sasa kugombea tena urais.


Serikali ya Burundi imepinga ukosoaji wa kimataifa kuhusu rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu, na kusema kuwa uamuzi wa rais haupaswi.
"kujadiliwa". Msemaji wa serikali ya Burundi Bw. Philippe Nzobonariba amesema, Burundi inafuatilia shughuli za kidiplomasia zinazoendelea ambazo zinaelekea kuharibu na kupaka matope mfumo na katiba ya nchi hiyo. Ameongeza kuwa shughuli kuhusu mamlaka, katiba na sheria haziwezi kujadiliwa, na hizo ni pamoja na rais Nkurunziza kugombea urais mwezi Juni, maandamano aliyoyataja ya haramu yanayoendelea na mchakato wa uchaguzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment