Image
Image

Serikali ya Tanzania yapiga marufuku matumizi ya mifuko kuhifadhia chakula*Yasema ina madhara makubwa.


Serikali  imewataka wananchi kuacha kutumia mifuko ya Plastiki  kuwekea  au kuhifadhia  chakula  kutokana na madhara  yanayoweza   kuwapata   badala yake  watumiye  vifungashio  vya  Glas  Chuma  isiyoshika kutu  na vyombo vingine  vya asili.
Hayo yamesemwa  Bungeni na Naibu  Waziri wa  Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais  Mazingira STEPHEN MASELE alipokuwa  akijibu  swali la  mbunge MKIWA  ADAM  KIMWANGA   aliyetaka kujua serikali   inachukua hatua  gani  kudhibiti  matumizi  ya  mifuk o  ya  plastiki ambayo kitaalam inaonekana kuwa na  madhara.
Waziri MASELE  amekiri  kuwa mifuko Plastiki  inaweza  kusababish a  madhara kwa kuweka chakula kutokanana  kemikali  zilizotumika  kutengeneza  mifuko hiyo  kuingia kwenye chakula na kukifanya  kuwa sumu.
Amesema  serikali imepiga  marufuku  matumizi  ya  mifuko hiyo  yenye unene  wa chini ya  Maikroni  30 na kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala.
Bangladesh imepitisha sheria.
Nchi ya kwanza kukataza mifuko ya rambo kutumika ni Bangladesh kwa sheria iliyopitishwa huko mwaka 2002.. California nako walipitisha Sheria hiyo mwaka 2012-13 na mpaka sasa hakuna sehemu utaenda California alafu ukawekewa kitu kwenye mfuko wa rambo.
Mwaka 1992 Singapore ilipitisha sheria iliyokataza kuuza ama kusafirisha big g kwa nchi yoyote duniani, ila big g zitengenezwe kwa ajili ya kulika na kununuliwa na raia wa Singapore tu. Baada ya miaka 12 yalifanyika mabadiliko na kuruhusu watu wa Singapore kununua big g ambazo hazina sukari yani Sugar-free chewing gums ambazo ni nzuri kwa meno na kinywa cha binadamu. Kwa sasa utaratibu uliopo ukikutwa unatema big g chini au unatafuna ovyo unapigwa faini.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment