Kukumbatiwa kwa kocha huyo kuna kuja baada ya Kamati hiyo ya TFF kudai kwamba, baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha huyo apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.
"Kwa niaba ya kamati ya utendaji Malinzi amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya COSAFA," alisema Msemaji wa TFF Baraka Kizuguto.
Alisema hatua hiyo ilifikiwa katika kikao cha kamati
ya utendaji kilichopokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.
Kizuguto alisema maamuzi hayo yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa, ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.
Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006-2012.
Pia katika kikao hicho kilichofanyika juzi, Kamati ya Utendaji ilipitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi.
Kizuguto alisema Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti izisisitize klabu za Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za klabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.
Pia kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.
Vile vile kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji kwa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.

Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa tume hiyo ambao ni
Tido Mhando ambaye ni Mwenyekiti, Deogratius Lyatto (Makamu Mwenyekiti),
Ephraim Mafuru (mjumbe), Beatrice Singano (mjumbe), Joseph Kahama (mjumbe) na
Ayoub Chamshana (mjumbe).
Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa mfuko huo.
Na kuhusu ajira Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia Juni Mosi, mwaka huu.Wambura kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa mashindano TFF.
Pia TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.
Vile vile Kamati ya utendaji imemteua Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashindano TFF.

0 comments:
Post a Comment