Image
Image

Yanga kuanza mazoezi Juni 8.


MENEJA wa klabu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, Hafidhi Salehe amesema kuwa kikosi chao kinatarajiwa kuanza mazoezi Juni 8, mwaka huu katika viwanja vya shule ya sekondari Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Kikosi hicho kitaingia kambini mara baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Hans Van de Pluijm kuwasili akitokea mapumziko.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa timu yao iko katika mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom.
Alisema mazoezi hayo yatakuwa maalumu kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame yanayotarajiwa kuanza Julai, mwaka huu.
"Timu yetu itaingia kambini mapema ili kujiandaa na kombe la Kagame, kwani lengo letu ni kuhakikisha kombe linabaki nyumbani," alisema Hafidhi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment