Ikiwa ni masaa kadhaa yamepita toka msanii wa filamu
nchini Kajala Masanja kufunguka ya moyoni juu ya Wema Sepetu na Petit Man na
kueleza kuwa kamwe katika maisha yake ya hapa Duniani hawezi kusahau fadhila na
moyo wa upendo ambaoulioneshwa na watu wao kipindi ambacho alikuwa na matatizo
na jinsi walivyoweza kujitolea mpaka kufikia hatua ya kuweza kumsaidia katika
matatizo ambayo alikuwa anakabiliana nayo kwa kipindi kile.
Kajala alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa
Instgram na ndipo hapo alipoamsha hisia za mashabiki ambao wameanza kumuomba
Wema Sepetu kumsamehe Kajala ili waweze kumaliza tofauti zao ambazo wanazo
sasa.
"Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya
ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema
kutoka moyoni mwangu.. najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na zaidi sana
mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo
wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo na mboni kubwa
katika kuokoa maisha yangu..
Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia
bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu..nakumbuka sana
mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili
yangu, mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu
mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu
ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu.
leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa Umma na
zaidi kwa mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote
mliyofanya juu yangu.. nawaombea kwa mungu muendelee na moyo huo huo kwani
naamini kuna wengi bado wanawategemea ili kukomboa maisha yao kwa wakati
aliyopanga Mungu. hata kitabu cha dini kilisema kuwa "huwezi kumpenda
mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" najua siku moja
tutaishi kama zamani.." Aliongeza Kajala
Baadhi ya mashabiki wameonesha kupenda jambo ambalo
limefanywa na Kajala na kuona kuwa amefanya jambo la kiungwana sana na
anastahili pongezi au msamaha kama kweli kuna jambo alitenda ambalo ndilo
limeleta utofauti wao ndiyo maana mashabiki hao wamemtaka Wema Sepetu na Martin
Kadinda kuweza kumsamehe ili waweze kuishi kama ambavyo walikuwa wakiishi
mwanzo.
"Mwantumum Kilindi: Good sana my Kajala
nimeipenda Allah atawasaidia mtaishi kama zamani mwenyezi Mungu kasema mara
saba sabini na inapendeza binadam kushirikiana si unafiki binadamu haipendezi
kununiana maana kila binadamu ataoza leo hii usimchukie binadamu mwenzako kwa
kosa gani haswa lisilo sameheka minatafurahi endapo mtapatana wote na Aunt Wema
na wewe Kajala ila marafiki sikuzote si wakumueleza undani wako namkishakua
marafiki wa tatu ni unafiki utaendelea nawapenda wote, sote tutafukiwa hujui
nani atatangulia leo hata kesho allah atawaongoza."
"Irene.Kimenye: Binadamu wote ndugu mlisahau
kabisa kwamba ninyi ni kioo cha jamii nakumbuka kwenye kipindi cha mkasi
ulichohojiwa ulikiri Wema ndiye aliyekufundisha biashara na mambo ya mtandao.
Urafiki wenu watu wengi nikiwemo mimi niliupenda lakini haukufika popote
mlichogombana mnakijua ninyi.Kama umekaa na ukafikiria na ukaona haya
uliyoyaandika hakika Mungu atawaongoza na mtarudi kama zamani ingawa sio kwa
ukaribu ule.
"Emelinaswebe: Wema msamehe mwezio jamani,haya
ni maisha tu yanapita, mnabidi mmalizane"
"Jasleeee_ safi sana Kajala Mungu ni mwema siku
zote amini kila jambo linasababu kwa Mungu. amini utayaweza yote katika yeye
akupae uzima. hivyo iko siku wema atakusamehe na mtaendelea kama zamani kwani
hizo nitofauti tu za kawaida mpendwa."
"Ajumysalum: Jamani huu ndiyo ungwana Kajala
hongera sanaa @wemasepetu @new_kajala samehaneni bhana asante @ my shoga
@pendojerry for the tag imenifunza kitu hii.


0 comments:
Post a Comment