Mshauri wa operesheni na
sheria za wakimbiz UNHCR Profesa Bonaventure Rutinwa
amesema hayo wakati akitoa semina kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
wa Kagera ambapo amewataka wakazi wa mkoa wa kagera na kigoma kutoa taarifa
haraka pindi wanapo ona dalili za wakimbizi wanaoingia nchini bila ratibu
maalumu nakuwataka wasiwahifadhi wakimbizi majumbani mwao badala
yake watoe taarifa kwenye mamlaka husika kwaajili ya kuepuka madhara
mabalimbali ikiwemo maradhi ambayo yaneweza kujitokeza.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalam ambae pia ni mkuu wa mkoa wa kagera John
Mongera amesema serikali imelipokea hilo na italishughulikia kwa kutoa elimu
kwa wananchi wa mkoa huo juu ya madhara ya kuwapokea na kuhifadhi wakimbizi bila
utaratibu na kuongeza wakimbizi wanapokelewa kwa kufuata kanununi na sheria
zilizoweka na umoja wa mataifa nakwamba serikali ya mkoa wa kagera imekwisha
pokea wakimbizi miasita ambao sasa wamesafirishwa na kupoelekwa
katika kambizi za wakimbizi zilizopo mkoani kigoma.
Hali hiyo imejitokeza mara
baada ya vuguvugu la machafuko linaloendelea huko nchini burundi ambapo
sasa kumekuwa na wimbi la wakimbizi wanaoingia nchini bila utaratibu ambapo
shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limelazimika kukutana na kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera kwaajili ya kujadili namna ya
kukabiliana na tatizo hilo.


0 comments:
Post a Comment