Image
Image

Viwanja 291 vyatangazwa kwa uwekezaji wa viwanda wilaya ya Kisarawe.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi mji wa Kisarawe utakavyojengwa, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe na Katibu mkuu wa kamati kuu ya Miradi,Mwanamvua Mrindoko na kushoto  ni Afisa Mradi wa Maliasili wa Wilaya ya Kisarawe,Cheyo Nyegele.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe  wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa  Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika  ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,ambapo wilaya ya Kisarawe inatarajia kuuza viwanja zaidi ya 291 kwa wewekezaji wa viwanda.
                             Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa  kazini
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali sambamba na Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika  ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakisoma vipeperushi vinavyoeleza namna ya mji wa kisarawe utakavyojengwa.
 Dar es Salaam.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe imetangaza viwanja 291 vilivyopimwa  kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda katika Wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Adamu Ng’imba amesema Halmashauri ya Kisarawe ina mazingira rafiki kwa uwekezaji wa viwanda kutokana na maeneo hayo yalivyopimwa.
Ng’imba amesema kuwa mradi wa viwanja hivyo umeshirikisha
wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na migogoro baina ya wawekezaji na wananchi ili kuepuka malengo yaliyokusudiwa yasifanikiwe.

Amesema katika viwanja vilivyopo katika mradi wa viwanda asilimia 63 ya fedha zitazopatikana katika uuzaji wa kiwanja zitakwenda kwa mwananchi ni katika kuepuka migogoro hiyo. Amesema wawekezaji baada ya kukamilisha taratibu zote za umiliki wa ardhi ni miaka mitatu kama ameshindwa kuendeleza Halmashauri
itachukua na kuuza kwa mtu mwingine.

Ng’imba amesema katika kuondokana na migogoro na ujenzi holela,Halmashauri imeamua kushirikisha wananchi katika maeneo husika. Amesema watakaopata maeneo ya uwekezaji katika Halmshauri ya Kisarawe watapata hati ndani ya siku saba na wananchi ndiyo watakaonufaika na mradi huo.
Crdt.Michuzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment