Image
Image

Watu 21 wameuawa wengine 81 wamejeruhiwa baada ya mhanga wa kutoka kikundi cha wapiganaji cha dola la kiislamu kulipua bomu.

Mhanga wa kutoka kikundi cha  wapiganaji cha dola la kiislamu  amelipua bomu alilokuwa nalo  katika msikiti kwenye jimbo la mashariki nchini saudia arabia na kuua watu 21 na kujeruhi wengine 81.

Taarifa zinasema kuwa mhanga huyo alikuwa amevaa bomu hilo ndani ya nguo zake na aliingia katika msikiti wa madhehebu ya Sunni na kujifanya kama ameenda kuswali swala ya ijumaa ya kutekeleza  unyama huo.

Mauaji hayo yanahusishwa na harakati za kikundi cha dola ya kiislamu kupinga mashambulizi ya majeshi ya Saudia Arabia katika nchi  ya Yemen dhidi ya waasi wa kikundi cha Houthi kinachoingoza kimabavu Yemen.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment