Image
Image

Zuma atoa wito wa kuwepo mshikamano zaidi Afrika


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa wito wa kuwepo kwa  umoja na mshikamano zaidi barani Afrika ili kulifanya bara hilo liwe na matumaini kwa vijana na vizazi vijavyo. Katika hotuba ya kuadhimisha Siku ya Afrika mjini Pretoria, Rais Zuma amesema siku hii ni ya kutazama mambo ya mbele na kutathmini changamoto zilizopo barani humo.
Rais Zuma akiwahakikishia wageni kutoka nchi mbalimbali za Afrika usalama wa kuishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini amesema, wananchi wa Afrika Kusini na raia wa kigeni waliotoka nchi zingine za Afrika kutafuta fursa nchini humo wamekuwa na mshikamano, na wanapaswa kuendelea na umoja huo kwa amani. Zuma amesema Siku ya Afrika pia ni kumbukumbu ya namna Afrika Kusini ilivyopokea msaada na mshikamano kutoka nchi zingine za Afrika wakati wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi. Akiashiria migogoro iliyopo katika nchi kadhaa za Kiafrika, Rais wa Afrika Kusini pia amesisitiza kuhusu umuhimu wa matatizo ya Waafrika kutatuliwa na Waafrika wenyewe.
Maadhimisho haya ni ya 52 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika OAU mwaka wa 1963.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment