Kulingana na toleo la kwanza la tathmini
ya kikanda kuhusu kutokuwa na uhakika wa chakula barani Afrika mwaka 2015,
Angola, Djibouti, Cameroon, Gabon, Ghana, Mali na Sao Tome na Principe
zimetimiza lengo la milenia la kupunguza kwa nusu idadi ya wenye lishe duni na
lile la Mkutano wa Dunia kuhusu Chakula la kupunguza kwa nusu idadi ya wenye
njaa.
Afrika Magharibi hasa imeonyesha kupiga
hatua kwa kupunguza kuenea kwa lishe duni kwa asilimia 60 katika ripoti ya
tathmini hiyo ya Shirika la Chakula na Kilimo, FAO.
Akizungumza kuhusu ripoti hiyo, Bukar
Tijani ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa FAO na Mwakilishi wake kwa
ukanda wa Afrika, amesema kuwa idadi ya wenye njaa imepungua kwa milioni 11
ukanda wa Afrika Magharibi, licha ya kuongezeka idadi ya watu kwa kasi na ukame
wa mara kwa mara katika nchi za Sahel.
0 comments:
Post a Comment