Saad Kawemba, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Azam FC, alisema jijini
Dar es Salaam jana kuwa hawajaipa kipaumbele michuano hiyo kwa sababu
nguvu kubwa wameiweka katika kusuka kikosi kwa ajili ya msimu wa 2015/16
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho
barani Afrika mwakani.
Alisema kikosi chao kitashiriki Kombe la Kagame, lakini michuano
hiyo ni sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya msimu mpya wa VPL.
Alisema sehemu kubwa ya kikosi chao itaundwa na wachezaji vijana na
wakubwa wachache ambao hawakuitwa kwenye timu zao za taifa ili kutoa
nafasi ya kupumzika kwa wale waliokuwa wanazitumikia timu zao za taifa.
“Maandalizi yanaendelea vizuri, tunaingia katika michuano mikubwa
ya Kombe la Kagame tukiwa tumefanya maandalizi ya wiki tatu tu. Katika
sayansi ya michezo hatuko 'fiti', ili uwe vizuri, lazima ufanye mazoezi
walau kwa wiki saba hadi nane," alisema Kawemba na kueleza zaidi:
"Tutatumia wachezaji wachache wa kikosi chetu cha kwanza kwa sababu
tutatoa mapumziko kwa wachezaji walioitwa kuzitumikia timu zao za
taifa. Kumbuka Azam ina wachezaji 12 Taifa Stars na hawajapata muda wa
kutosha wa kupumzika tangu kumalizika kwa msimu uliopita.
“Kombe la Kagame kwa kweli siyo ‘priority’ (kipaumbele) yetu,
tunaomba radhi kwa waandaaji wa mashindano hayo. Tutacheza, lakini
tutashiriki kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao."
Aggrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Brian Majwega, Salum
Abubakar 'Sure Boy' na Frank Domayo ni miongoni mwa nyota wa Azam FC
watakaoikosa michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es
Salaam mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment