Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine mjini Mbeya juzi, Malinzi ambaye yupo mjini hapa kwa ziara na
timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15, alisema kuwa kila
mkoa (chama cha soka cha mkoa husika) nchini umeagizwa na shirikisho
hilo kuwa na kituo kimoja cha michezo ambacho TFF itahakikisha
inakisaidia kuwa na walimu wa kutosha, vifaa na mahitaji mengine.
Malinzi pia alisisitiza kuwa shirikisho hilo litasimamia ipasavyo
kanuni ya kila timu ya ligi kuu nchini kuwa na timu ya vijana
itakayokuwa inacheza mechi za utangulizi ikiongozwa na kocha mwenye
taaluma stahiki.
Malinzi aliongeza kuwa ya timu ya taifa ya vijana iliyopiga kambi jijini hapa itafanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
Alisema mwezi ujao itaelekea visiwani Zanzibar, Agosti itakuwa
Mwanza, Septemba itakuwa Morogoro na Oktoba itakuwa Arusha huku
ikiendelea kuchujwa na Desemba itafanya ziara katika nchi za Malawi,
Zambia, Botswana na Afrika Kusini kabla ya kuelekea Kaskazini mwa
Afrika.
Malinzi alisema wanaamini maandalizi hayo yatatoa timu bora ya
vijana itakayoiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya kimataifa
ikiwamo Olimpiki na fainali za Kombe la Dunia 2026.
"Ni vigumu sana timu kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa
maandalizi ya muda mfupi. Maandalizi tunayofanya tunaamini yatatusaidia
kuimarisha timu yetu kwa ajili ya miaka ijayo,” alisema Malinzi.
Katika ziara yake jijini hapa, timu ya taifa ya vijana ya U15
ilicheza mechi ya kirafiki na kushinda 3-0 dhidi ya timu ya Mbeya
Combine ya umri huo mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment