Kocha mkuu wa Taifa Stars,
Boniface Mkwasa, alisema kwamba mazoezi ya kikosi hicho yanaendelea
vyema.
Alisema kwamba wachezaji watakaosafiri kuelekea Kampala Alhamisi
watajulikana baada ya mazoezi ya mwisho kesho jioni na yatatokana na
ripoti ya daktari wa timu hiyo.
"Najua kila mmoja anahitaji kuona tunavuna matokeo mazuri,
wachezaji wanajua na sisi makocha tunajua kiu waliyonayo mashabiki,"
alisema kocha huyo ambaye bado pia anaifundisha Yanga kama kocha
msaidizi.
Kikosi cha Stars kimeweka kambi yake mjini Bagamoyo, mkoani Pwani
na kinafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani huku benchi la
ufundi likiruhusu mashabiki kuangalia mazoezi hayo.
Alisema lengo la kuwaweka nje ya mji ni kuwapa muda wa kupumzika na kufikiria mazoezi tu.
Wachezaji walioitwa katika kikosi cha Stars na wanaendelea na
mazoezi ni pamoja na Mwadini Ally wa Azam, Ally Mustapha 'Barthez'
(Yanga), Mudathir Khamis (KMKM), Shomari Kapombe (Azam), Michael Haidan
(Ruvu Shooting), Mohammed Hussein (Simba), Mwinyi Hajj (KMKM), Kelvin
Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Abdi
Banda (Simba) na Simon Msuva wa Yanga.
Wachezaji wengine ni Said Ndemla, Ramadhan Singano 'Messi' (Simba),
Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam), Atupele Green (Kagera
Sugar), Rashid Mandawa (Mwadui), Ame All (Azam), Deus Kaseke (Yanga),
Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Mudathir Yahya wa Azam.
CANNAVARO NJIA PANDA
Nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro', ameliambia gazeti
hili jana jioni kwamba anatarajia kuanza mazoezi mepesi leo jioni na
hatima yake ya kusafiri kuelekea Kampala haijajulikana.
Beki huyo wa kati na nahodha wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara
alisema kuwa mahali alipochanika (juu ya jicho), kidonda kinaendelea
vizuri kutokana na madaktari wake kumshona 'kisasa'.
"Kidonda kinaendelea vizuri, siku hizi madaktari wanashona vizuri,
ila kesho (leo) ndiyo nitaanza mazoezi mepesi na daktari ndiye atasema
kama ninaweza kucheza Jumamosi," aliongeza Cannavaro.
Alisema eneo lililochanika ni palepale alipoumia katika mechi iliyopita dhidi ya watani zao, Simba na ameshonwa nyuzi tano.
Cranes itashuka uwanjani Jumamosi kurudiana na Stars ikiwa
imeshatanguliza mguu mmoja katika fainali hizo za CHAN baada ya
kuisambaratisha Stars kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar
Juni 20, mwaka.
0 comments:
Post a Comment