Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Julius
Malaba alisema maombi ya waangalizi wa ndani wa uchaguzi yalishapokewa
huku mchakato wa kuwateua wanaostahili ukiendelea kufanyika.
“Waaangalizi wa ndani wa uchaguzi wameshatuma maombi yao na mchakato wa kuzipata taasisi zenye sifa ya kuwa waangalizi unaendelea muda utakapofika zilizochaguliwa zitatangazwa,” alisema.
Kuhusu waangalizi wa nje, Malaba alisema jukumu hilo linatekelezwa
na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa na kwamba
jumuiya kadhaa zimeshatumiwa mialiko.
“Unapomwalika mtu ama taasisi haimaanishi lazima aje, uamuzi wa kuja ama kutokuja unabaki kuwa ni hiyari ya mhusika,” alisema.
Hata hivyo, jitihada za kumpata Waziri wa wizara hiyo, Bernard
Membe, kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa kutokana na simu yake ya
kiganjani kutopatikana.
Membe ni miongoni mwa mawaziri katika serikali ya Rais Jakaya
Kikwete, wanaoomba kuteuliwa na CCM ili wawanie urais katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka huu.
Kuhusu changamoto zinazotokana na uandikishaji wapiga kura kwa
mfumo wa BVR, Malaba alisema Nec mchakato huo umeahirishwa kwa mikoa
kadhaa ukiwamo Dar es Salaam ili vifaa vilivyokusanywa katika mikoa
ambayo mchakato umemalizika viweze kutosheleza idadi ya wakazi wake.
“Tumejipanga kuhakikisha wakazi wote wa Dar es Salaam wanaandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura ndio utaona tumesogeza mbele siku ya uandikishaji ili kukusanya vifaa vyote vilivyotumika katika mikoa mingine kuendana na idadi ya watu,” alisema.
Pia, Malaba alisema hadi sasa hakuna tarehe mahususi ya mwisho ya
kuzaliwa kwa mpiga kura mwenye sifa ya kujiandikisha, isipokuwa ni
atakayekuwa na umri wa miaka kuanzia 18 ifikapo Oktoba 25, 2015.
0 comments:
Post a Comment