Hadi kufikia mwisho wa uhai wake, Bunge hilo lililoongozwa na Spika
Anne Makinda
(Pichani), na Naibu Spika Job Ndugai, litakuwa limefanya
mikutano 20 huku vikao vya mwisho vikiwa ni 38.
Ratiba ya nyongeza iliyotolewa jana na ofisi ya Bunge baada ya
kikao cha Kamati ya Uongozi, ilionyesha kuwa Rais Jakaya Kikwete
atalivunja Bunge hilo baada ya kulihutubia.
Pamoja na tukio hilo la kihistoria, Bunge limejadili miswada
mbalimbali ikiwamo (iliyopitishwa) ya sheria ya fedha ya mwaka 2015,
sheria ya vituo vya pamoja mipakani ya mwaka 2015 na sheria ya kufuta
sheria ya benki ya Posta ya mwaka 2015.
Aidha, baada ya maoni ya wadau wa habari, muswada wa haki ya kupata
habari ambao ulikuwa ujadiliwe Juni 27, mwaka huu, baada ya kusomwa kwa
mara ya kwanza, uliondolewa bungeni hadi serikali ijayo.
Miswada inayoendelea kujadiliwa ni muswada wa sheria ya masoko ya
bidhaa wa mwaka 2015, muswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za
uhalifu na mashahidi wa mwaka 2015.
Mingine ni muswada wa sheria ya Petroli wa mwaka 2015, muswada wa
sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 20q5, muswada
wa sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya
mwaka 2015.
Ratiba hiyo imeonyesha kuwa muswada mwingine nj wa sheria ya Tume ya walimu wa mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment