Akiifunguwa
Semina ya usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hapo
kwenye ukumbi wa Baraza hilo Mbweni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi alisema tabia ya baadhi ya viongozi kuwaombea Vijana wao
kuwachiliwa kwa makosa yao ya makusudi ni kuwavunja moyo Polisi na kupelekea
kuonekana hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
Balozi
Seif alisema imekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa kwa baadhi ya Viongozi
kuwaombea vijana wao wasifikishwe Mahakamani wakati
wanapofanya makosa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaondosha heshima yao
ndani ya jamii.
Alisema
uvunjwaji wa sheria za usafiri wa barabarani unaofanywa na watumiaji wa
barabara hizo kama waendesha vyombo vya moto, gari zinazobururwa na wanyama,
baskeli na ha waendao kwa miguu husababisha ajali zinazoleta
madhara kwa Taifa.
Balozi
Seif alieleza kwamba Serikali imejenga bara bara mbali mbali Nchini lwa lengo
la kuimarisha miundombinu ili kuufanya usafiri huo kuwa salama kwa watumiaji,
lakini kwa bahati mbaya kuimarika huko kumekuwa ndio sababu ya waenesha vyombo
vya moto kwenda mwendo wa kasi katika barabara hizo bila ya kujali watumiaji
wengine wa bara bara
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwamba hivi sasa ipo tabia ya hatari kwa
vijana waendeshao vyombo vya moto vya ringi mbili kufanya mashindano yasio
rasmi katika bara bara mbali mbali hasa zilizomo ndani ya maeneo ya Mji wakiwa
katika mwendo wa hatari wa kasi kubwa.
Alisema
jamii imekuwa shahidi iliwaona Vijana wanaoendesha Vyombo vya ringi mbili Vespa
na Pili pili wakipakizana watu zaidi ya wawili katika chombo huku wakifukuzana
kwa mwendo wa kasi wakiwa wamekaa katika mkao wao maarufu { T. ONE
} huku vyombo hivyo vikichomolewa breki kwa makusudi.
Alisema
chakusikitisha zaidi baadhi ya vijana hao huendesha vyombo hivyo kwa ringi moja
tuu vikiwa kwenye mwendo mkali bila ya hata kuvaa kofia ngumu lakini
jambo la ajabu zaidi baadhi yao ni viongozi katika Jamii hii.
Alifahamisha
kwamba matatizo ya usalama katika bara bara yanamgusa kila mwana Jamii, hivyo
ni wajibu wa kila Mwananchi kusaidia kuchangia upatikanaji wa ufumbuzi wa
kudumu ili kuifanya sekta hiyo kuwa salama kwa watumiaji wote wa Bara bara.
“ Usafiri wa bara bara kuwa salama katika visiwa vya Zanzibar kutaimarisha uchumi wake kwa kuitumia miundombinu ya usafirishaji ambayo inajengwa kwa kutumia fedh nyingi pamoja na kuiokoa nguvu kazi ya Taifa inayohitajika katika uzalishaji “. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia
usumbufu wa tatizo la vituo vya dala dala katika baadhi ya maeneo ya Mji wa
Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi kuendelea
kuwa wastahamilivu wakati Serikali yao ikiwa katika harakati za kuimarisha
mpango Mkuu wa Mji wa Zanzibar.
Alisema
mp[ango huo utaweka utaratibu mzuri wa vituo vya gari za abiria utakaorahisisha
usafiri kwa Wananchi hasa wale wanaoonekana kusumbuka kwa kukosa kituo cha
uhakika cha wananchi wanaosafiri na kurejea Zanzibar kwa kutumia Bahari ambao
hulazimika kubeba mizigo yao kwa kufuata kituo cha gari masafa marefu.
Balozi
Seif alizishauri Taasisi zinazohusika na usafiri, mipango Miji na Vijiji kufikiria
njia bora za mpito zitakazosaidia wananchi kuondokana na usumbufu wanaoupata wa
usafiri hususan katika Miji ya Zanzibar.
Kuhusu
tabia mbaya ya baadhi ya madereva wenye tabia ya kuwachukuwa abiria na
kutowafikisha sehemu zilizowekwa kisheri Balozi Seif aliwashauri Wananchi
kutokubali kuteremshwa njiani na ye yote atakayefanyiwa hivyo aripoti Polisi
ili Dereva atakayehusika na tatizo hilo achukuliwe hatua za kisheria.
Alisema
limekuwa ni jambo la kawaida kwa madereva wad ala dala na hata gari za shamba
kuchukuwa abiria na kuwakatisha safari zao hali inayosababisha usumbufu mkubwa
kwa abiria hao wakati wengine wanaelekea Hospitalini.
Balozi
Seif alifahamisha kuwa gari yoyote inayoingizwa katika shughuli za
biashara inalazimika kufuata sheria na taratibu za biashara husika kinyume
chake ni kufanya makosa.
“ Dereva anapoanza kazi ya kupakia abiria aelewe kuwa ameingia katika mkataba na abiria. Hivyo anawajibika amchukuwe na kumfikisha hadi kituo cha mwisho cha safari iliyopangiwa dala dala yake abiria huyo ambaye naye atawajibika kulipa Nauli kwa huduma aliyopewa. Mmoja wao kama hakutekeleza hayo atakuwa amefanya kosa na anastahiki kuchukuliwa hatua za kisheria “. Alisema Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wananchi kwambacSerikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inaungana na Umoja wa Mataifa katika kuona kwamba ifikapo
mwaka 2020 vifo vinavyotokana na ajali bara barani vinapungua kwa asilimia 50%.
Balozi
Seif alieleza kuwa katika kutekeleza hilo Serikali imeunda kamati ya Kudumu ya
Kitaifa ya usalama bara barani kama watendaji wa miundombinu, afya,
Elimu, Polisi na Jumuiya za Magari ambayo itakuwa na jukumu la kutekeleza
jukumu hilo.
Mapema
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mh. Juma Duni Haji alisisitiza
umuhimu wa mashirikiano ya pamoja kwa Taasisi zote zinazosimamia shughuli
na harakati za Bara bara ndio njia pekee itakayosaidia kupunguza au kuondosha
kabisa changamoto ya usafiri wa Barabarani.
Mh.Juma
Duni alishauri kwamba ni vyema inapotokea changamoto ya usafiri wa Barabarani
washirika wa Taasisi zinazohusika na Sekta hiyo wakajenga utaratibu wa kukutana
mara kwa mara katika njia ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.
Wakitoa
mada kwenye semina hiyo ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu usafiri na
usalama Barabarani Mkurugenzi wa Idara ya usafiri na Leseni Nd. Suleiman
Kirobo, Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Msaidizi Kamishna wa Polisi ACP
Nassor Ali Moh’d pamoja na Mdau wa Sekta ya Usafiri Bwana Waziri Hashim
walisema zipo sheria zilizopitwa na wakati mabazo kutofanyiwa marekebisho ya
haraka zitaendelea kuchangia matatizo yanayopatikana katika matumizi ya usafiri
wa Bara barani.
Waliitaja
tabia iliyozuka hivi sasa kwa madereva wa vyombo mbali mbali vya moto kutumia
simu za mikononi wakati wanaendesha vyombo hivyo wanalipa changamoto kubwa
jeshi la Polisi usalama bara barani katika kukusanya ushahidi wa makosa kama
hayo.
Watoa
mada hao walisema ili kudhibiti hali ya usalama kikamilifu umefika wakati kwa
sasa Bara bara za hapa nchini kulindwa kwa mitambo maalum ya kisasa ya
Camera za CCTVG mfumo ambao hutumiwa na Miji mikubwa Duniani na kuleta
mafanikio mazuri.
0 comments:
Post a Comment