Wizara ya afya nchini Saudi Arabia, ambako
ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza, imesema kesi sita za maambukizi ya
ugonjwa huo zimeripotiwa katika mji wa Hofuf ulioko mashariki mwa nchi hiyo,
huku wagonjwa wawili wakiwa na hali mbaya. Wizara hiyo imesema, wagonjwa hao
walikuwa na mawasiliano na watu wanaoshukiwa kuwa na MERS au waliothibitishwa
kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
Nchini Oman, mtu mmoja mwenye umri wa miaka
75 aliyekuwa akisumbuliwa na kichomi na homa kali, amethibitishwa kuwa na
virusi vya MERS, na kwamba anaendelea vizuri.
Shirika la Afya Duniani limesema, dalili za
ugonjwa huo ni homa, kukohoa, na kuishiwa pumzi, na unaweza kusababisha kichomi
na figo kushindwa kufanya kazi.
0 comments:
Post a Comment