Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban
Ki-moon amesema kasi ya matumizi ya
maliasili ya kimaumbile imezidi kwa kiasi kikubwa uwezo wa sayari ya dunia wa
kuzalisha maliasili hizo kwa njia endelevu, hivyo binadamu wanatakiwa
kubadilisha muundo wa matumizi wa sasa haraka iwezekanavyo.
Bw. Ban Ki-moon aliyasema hayo jana kwenye siku
ya mazingira duniani. Amesema kuwa, lengo la maendeleo endelevu ni kuinua ubora
wa maisha ya watu wote kwenye msingi wa kutosababisha uharibifu kwa mazingira,
na kutoharibu mahitaji ya vizazi vijavyo kwa maliasili.
Amesema, ili kutimiza lengo hilo, tunatakiwa
kubadilisha muundo wa matumizi, kwa kupunguza matumizi ya nishati, maji na
rasilimali nyingine, na kutunza chukula.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment