Kabla ya hapo,
kundi la Daesh ambalo linafanya jinai nyingi katika nchi za Iraq na Syria
liliwataka wanamgambo wa Taliban wajiunge na kundi hilo.
Inafaa kukumbusha pia
kuwa, katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, kumetokea mapigano kadhaa baina
ya kundi la Taliban na lile la Daesh huko Afghanistan.
Duru za kijeshi za
Afghanistan zimethibitisha habari za kutokea mapigano baina ya makundi hayo
mawili na kukanusha kuhusika jeshi la Afghanistan kwenye mapigano baina ya
makundi hayo.
Mwezi moja nyuma, Muhammad Hanif Atmar, mshauri wa usalama wa
taifa wa Rais wa Afghanistan aliliambia Baraza la Senate la nchi hiyo kuwa
kundi la kigaidi la Daesh ni hatari kubwa kwa Afghanistan na eneo hili zima
kwani kundi hilo lina nia ya kuingia kwenye nchi za Asia ya Kati kupitia
kaskazini mwa Afghanistan.
0 comments:
Post a Comment