Image
Image

Russia yarusha angani satalaiti ya kijeshi.


Jeshi la Russia limerusha kwa mafanikio satalaiti ya kijeshi katika anga za juu kwa kutumia roketi la Soyuz-2.1a na tayari satalaiti hiyo imeshaingia kwenye mzingo wa dunia.
Msemaji wa Jeshi la Anga la Russia, Kanali Dmirty Zenin amethibitisha habari hiyo na kongeza kuwa, satalaiti hiyo ilirushwa anga za juu jana Ijumaa katika kituo cha anga za juu cha Plesetsk.
Hii ni mara ya kwanza kwa kombora la Soyuz-2.1a kurusha satalaiti baada ya kufeli kombora hilo kurusha satalaiti ya mizigo ya M-27M mwezi Aprili.
Jaribio hilo lililoshindwa lilifanyika tarehe 28 Aprili katika kituo cha anga za juu cha Baikonur huko Kazakhstan.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment