Akizungumza kufuatia hafla ya uridhiaji huo
wa Niger, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Guy Ryder amesema anatumai nchi zaidi
zitauridhia ili uanze kuutekelezwa, akiongeza kuwa hatua ya Niger inawapa
matumaini mamilioni ya wanawake, watoto na wanaume ambao wamenaswa katika
utumwa wa kisasa.
ILO inakadiria kuwa kote duniani, watu
milioni 21 ni waathirika wa ajira za lazima, wengi wao wakinyanyaswa katika
kilimo, uvuvi, ajira za nyumbani, ujenzi, usindikaji, uchimbaji migodi na
nyinginezo.
Imeongeza kuwa wanawake na wasichana hasa
hukumbwa na unyanyasaji wa biashara ya ngono.
0 comments:
Post a Comment