Akiongea na waandishi wa habari mjiniNew
York msemaji wa Katibu Mkuu Stephanie Dujarric amesema kazi hiyo itafanywa
kundi la nje na huru lisilofungana na upande wowote .
''Mapitio yatachunguza namna ripoti ya ukatili huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ilivyoshughulikiwa na ukubwa wa masuala yanayohusiana na namna Umoja wa Mataifa unavyomaanisha katika kushughulika taarifa za jinsi hii.''
Bwana Dujarric amesema kuwa kama
ilivyoelezwa katika majuma ya hivi karibuni Katibu Mkuu anahuzunishwa kwa kina
na tuhuma za ukatili wa kijinsia CAR na namna pande mbalimbali za Umoja wa
Mataifa zilivyoshugulikia tuhuma hizo.
Amesema lengo la kutangazwa kwa mpango huo
ni kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa hautelekezi waathiriwa wa ukatili wa
kijinsia hususani pale ukatili huo unaopotendwa na wale wanaopaswa kuwalinda.
Kwa mujibu wa Dujarric, katika siku chache
zijazo watatangaza majina ya wanaoongoza mapitio na hadidu za rejea.
0 comments:
Post a Comment