Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto, UNICEF limesema lengo ni kubadili mwelekeo wa watoto kuacha kwenda
shule na badala yake waende na wasome kwa kuwa elimu ni haki ya msingi ya mtoto
bila kujali anaishi mazingira ya mzozo au la.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo mjini
Yambio, Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Kusini Jonathan Veitch amesema mzozo
unaoendelea unazidi kuzorotesha uchumi lakini elimu ni suala la uokozi wa
maisha kwa kuwa mtoto ambaye mama yake anajua kusoma ana uwezo wa kuishi zaidi
ya umri wa miaka mitano.
Hata hivyo mpango huo wa elimu Sudan
Kusini unakumbwa na mkwamo ambapo umechangia asilimia 21 tu kwa mwaka huu,
lakini serikali ya Japan imechangia dola Milioni 9.5 kusaidia miradi ya UNICEF
nchini humo ikiwemo ile ya elimu.
Kampeni hiyo ya kitaifa ya elimu imeanza
mwezi Februari ikilenga watoto 400.000, gharama yake ni dola Milioni 42 na
lengo la ni kuhakikisha watoto watoro shuleni wanarejea na wale ambao
hawakuwahi kwenda shule wanafanya hivyo hasa kwenye maeneo yenye mizozo.
0 comments:
Post a Comment