Wananchi
wa kijiji hicho wanasema wanawake na watoto ndiyo wanateseka zaidi na kwamba
wakifika katika zahanati hiyo hawapati huduma za afya badala yake wanapewa
karatasi kwenda kununua dawa.
Kwa hali hii wanadai imekuwa kero hali
ambayo inawakatisha tamaa ya kuendelea kuchagia fedha kwa ajili ya bima ya afya
na kwamba wameshatoa malalamiko ngazi ya wilaya bila mafanikio sababu ambayo kwa
sasa inayowalazimu kutembea umbali wa zaidi km 10 kutafuta huduma za afya.
Mganga wa zahanati ya kijiji cha kiti cha
Mungu Dkt.Chard Mshana amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa dawa
zinazoletwa katika kijiji hicho ni kidogo sana ikilinganishwa na idadi ya
wananchi wanaohitaji huduma za afya.
Akijibu malalamiko hayo mkurugenzi wa halmashuri
ya wilaya ya mwanga Bw.Jamuhuri Wilium ameahidi kufuatialia tatizo hilo na
kulitafutia ufumbuzi kwenye kamati za afya za wilaya ambazo zinahusika
kusambaza dawa katika zahanati .
0 comments:
Post a Comment