Wafugaji hao wenye ngo'mbe
Elfu-38 walifika Wilayani
Tunduru mwaka 2006 wakitokea Ihefu Mkoani Mbeya wanasema wao hawakataki kuhama
bali wanataka Serikali iwaon eshe
kwa kwenda .
Wafugaji hao wameamua kuandamana
hadi kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Tunduru kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ,Bwana FARIDU HAMIS kuwataka kuondoka ndani ya siku tatu .
Katibu wa Chama
cha Wafugaji Kanda
ya Kusini ,Bwana CORNERY KAPINGA
ameiomba Serikali kuwatengea maeneo
miongoni mwa mapori mengi katika Wilaya ya Tunduru .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru anayehamia Wilaya
ya Namtumbo , Bwana CHANDE BAKARY NALICHO ameoongeza muda wa wafugaji hao kuondoka kwenye maeneo tengefu na kando ya
Mto Ruvuma na wakitakiwa kufuata taratibu katika maeneo
watayokubaliwa na wanakijiji.
0 comments:
Post a Comment