Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo Rais Jacob
Zuma wa Afrika Kusini amesema nchi za Afrika zinatakiwa kuwawezesha vijana na
kuwashirikisha katika kufanya maamuzi, kwani hatua hiyo ni muhimu kwa
mustakbali wa Afrika. Rais Zuma amesema zama wazee pekee kuongoza zimepitwa na
wakati, na sasa ushiriki wa vijana unatakiwa kuonekana wazi.
Mwenyekiti wa baraza la uchumi wa Dunia Bw
Klaus Shchwab amesema Afrika ina nguvu kazi kubwa, na wengi ni vijana ambao
mwaka 2040 wanatarajiwa kuwa asilimia 50 ya vijana duniani.
0 comments:
Post a Comment