Matokeo yanaonyesha chama
hicho kimeshinda kwa asilimia arobaini na mbili ya kura, huku kikiwa na
upungufu wa viti kumi na nne kuweza kuunda serikali.
Huku kile kinachoungwa mkono
na wakurd cha HDP kikivuka asilimia kumi kwa kupata viti takriban themanini
hivyo kuweza kuingia bungeni kwa mara ya kwanza.
Iwapo itathibitishwa, matokeo
haya yanaashiria mwisho wa utawala wa miaka kumi na tatu wa chama cha AKP hali
itakayokwaza mipango ya rais Erdogan ya kumpa rais madaraka zaidi.
Baada ya kupiga kura yake
katikati mwa Uturuki katika mji wa Konya, waziri mkuu Ahmed Davutoglu aliongea
na waandishi wa habari, na kuwaeleza kwamba"natarajia mema kwa nchi yangu
na watu wangu. Leo niko hapa kama waziri mkuu kwa hiyo nina jukumu. Siku ya leo
ni ishara ya imani ya nchi yetu, kwa hiyo nataka kusema asanteni nyote ambao
mmeshiriki katika uchaguzi wa bila kujali uamuzi wenu."
0 comments:
Post a Comment