Image
Image

News Alert:Viongozi wa dini waombwa kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.


Viongozi  wa  dini  Mkoani  Arusha  wameombwa  kutumia  fursa  walizonazo  kusaidia  kuhamasisha  wananchi  kujiandikisha  kwenye  Daftari  la kudumu  la  wapiga  kura  na pia  umuhimu  wa  kupiga  kura hatua itakayosaidia  kuepusha  malalamiko  na  migogoro  isiyo ya  lazima  wakati  wa  uchaguzi .
Rai  hiyo imetolewa  na  Askofu  wa  Kanisa  la  International  Evangelisim  Centre ,Dakta   ELIUD  ISANGYA  alipokuwa  akizungumza  katika  ibada  maalumu  ya  kuhitimisha  mafunzo  ya  kwa  wachungaji   wa  kanisa  hilo  lililoko  Sakila  Wilayani  Arumeru .
Amesema  msaada  wa  viongozi  wa  dini  na  makundi  mengine  yenye  ushawishi   katika  jamii  unahitajika  sana  wakati  huu , ambao  nchi  inaelekea  kwenye  hatua   muhimu   ya  uchaguzi  mkuu   na  kwamba  kila  mmoja  akitimiza   wajibu  wake   matatizo na malalamiko  mengi yanayojitokeza  baada  ya  uchaguzi  yatapungua .
Baadhi  ya  wananchi   wakiwemo  waumini   wa  kanisa  hilo  wameiomba  serikali   kuendelea  kurekebisha  dosari  zinazojitokeza  wakati  wa  kujiandikisha  ili  kuwaepushia  wananchi  usumbufu  na  kupoteza  muda  mrefu   wakati  wa  kujiandikisha .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment