Mifuko ya jamii, mashirika yasiyo ya Serikali na wadau mba limbali wameombwa
kujitokeza kusaidia huduma za jamii
badala ya kuiachia serikali ambayo wakati mwingine inazidiwa na majukumu na
hivyo kuchelewesha maendeleo katika jamii.
Hatua hiyo imesababisha Mfuko wa Pensheni wa LAPF kutoa msaada wa
mabati wenye thamani ya Shilingi Milioni Nne ,kusaidia ujenzi wa maabara katika
Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi .
Afisa Mkuu wa mfuko huo ,ISAYA MWAKIFULEFULE amesema mchango huo ni sehemu ya faida ambayo
mfuko unairudisha kwa jamii .
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa , MSONGA
MATIKU akipokea msaada huo ametaka mifuko
mingine ya jamii pamoja na wadau
wengine kuiga mfano huo.
0 comments:
Post a Comment