Serikali kupitia mamlaka ya
chakula na dawa imesema katika mwaka 2014/15 imefuta usajili wa aina tatu za dawa
ikiwemo dawa ya malaria ya AMODIAQUINE, dawa ya fungus aina na Koteconazole
pamoja na dawa ya kikohozi ya zenye
kiambata aina ya PHENYLPROPANOLAMINE
baada ya kuonekana na madhara kwa maisha ya binadamu.
Akijibu swali la mbunge
wa TUNDURU KUSINI , MTUTURA ABDALLAH MTUTURA l ililoulizwa kwa niaba
yake mhe L EDIANA MNG'ONG'O Aliyehoji
kwanini serikali isijiridhishe map ema kabla ya kuruhusu dawa kutumika na baadae kuzipig a mafuruku kutokana na
kubainika kuwa na madhara kwa afya ya binadamu .
Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dakta
STEPHEN KEBWE amesema dawa zinazoingia
nch i ni hu fanyiwa
tathimini y a ubora, usalama na ufanisi wake na kiwanda
kukaguliwa kama kinatengeneza dawa kwa kufuata vigezo vya utengenezaji bora wa dawa.
Wakati huo huo, Serikali imesema
upembuzi yakinifu , usanifu wa kina na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili
ya ujenzi wa daraja la Momba linalounganisha Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Wilaya Momba kati ya vijiji vya
Kilyamatundu na Kamsamba umekamilika.
Akijibu swali la Mbunge wa Kwela,
IGNAS MALOCHA aliyetaka kujua ni hatua gani zimechukuliwa katika ujenzi wa
daraja hilo na lini ujenzi wa daraja hil o
utakamilika na kiasi cha fedha kinachohitajika.
Waziri wa nch i ,Ofisi wa Waziri
Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Elimu
MAJALIWA KASIM MAJALIWA amesema
serikali kupitia wakala wa barabara-TANROAD- inakamilisha maandalizi ili
kutangaza zabuni ya ujenzi.
Amesema ujenzi wa daraja hilo la
mto MOMBA unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2015/ 20 16 na ujenzi
unatarajiwa kuchukua takribani miaka mwili.
Bunge limeelezwa kuwa Serikali imetenga Shilingi
Milioni 150 katika mwaka wa fedha 2015/ 20 16 katika vyanzo vyake vya
mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga jumla ya mita za mraba elfu mbili ka tika
stendi ya mji mdogo wa Mbarar i na Shilingi Milioni 566.7 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa barabara katika mji huo.
Akijibu sw ali la mbunge Mbeya
vijijini, LUCKSON NDAGA MWANJALE Aliyehoji
serikali imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ahadi ya Rais aliyoitoa
wakati wa kampeni ya mwaka 2010 kuhusu ujenzi wa stendi Mba rar i na barabara
zake.
Naibu waziri MAJALIWA KASSIMU
MAJALIWA mesema kutokana na kupanda kwa
gharama za ujenzi tathimni iliyofanywa mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa jumla ya
shilingi bilioni 1.6 zitatumika kukamilisha ujenzi huo.
0 comments:
Post a Comment