Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Mleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, baada ya yeye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasili Kijiji cha Kyamkwikwi, wilayani Muleba mkoani Kagera leo, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa cha Bumbile wilayani Muleba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, jana, Juni 7, 2015. Picha na Bashir Nkoromo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi, baada ya kuwasili Kijiji cha Kyamkwikwi, wilayani Muleba mkoani Kagera leo, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa cha Bumbile wilayani Muleba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, jana, Juni 7, 2015. Picha na Bashir Nkoromo.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa gati katika ziwa Victoria, katika eneo la
Kyamkwikwi wilayani Muleba mkoani Kagera, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa
cha Bumbile wilayani Muleba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani
ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, jana, Juni 7, 2015. Picha na Bashir
Nkoromo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiielekeza boti eneo la kutia nanga ili Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wasafiri nayo kwenda Kisiwa cha Bumbile.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akipanda boti kutoka kijiji cha Kywamkwikwi kwenda Kisiwa
cha Bubile, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai
wa Chama mkoani Kagera, jana, Juni 7, 2015. Picha na Bashir Nkoromo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Nape (kulia) wakiwa na Profesa Anna
Tibaijuka wakati safari ilipoanza kwenda Kisiwa cha Bubile, Kinana akiwa katika
ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera,
jana, Juni 7, 2015. Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini, Mbunge wa Muleba Kusini,
Profesa Anna Tibaijuka, alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika
kijiji cha Katunguru, wilayani Muleba jana.
Katibu wa NEC, Itkadi
na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Kijiji cha Katunguru.katika
ziara ya Kinana mkoani Kagera, jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman
KinanaMbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa
Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera, jana, akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera.
wananchi wakifuatilia hotuba ya Kinana kwenyemkutano
huo, wa Mleba mjini mkoani Kagera.
Kagera.
Wavuvi katika visiwa vilivyopo
ndani ya ziwa Victoria upande wa mkoa wa Kagera wameitaka serikali kuacha
kuwanyanyasa kwa kuteketeza nyavu zao wakati inaruhusu nyavu hizo kuingizwa
nchini na wao kuuziwa madukani,bila ya wauzaji kuchukuliwa hatua za kukamatwa
kama wao.
Wavuvi hao wametoa malalamiko
hayo mbele ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi taifa Komredi Abdulrahman Kinana,kwenye
mkutano wa hadhara wa visiwa vya Bumbile,mazinga na iroba kabla ya kuwasili
kwenye mwalo wa katunguru wilaya ya muleba mkoani Kagera,ambapo wasema
wamechoshwa na vitendo hivyo,sanjari na vyombo vyao kukamtwa na sumatra na
kutozwa fedha bila kupewa risiti.
Akiwa katika wilaya ya Muleba
mkoani Kagera,kwenye mkutano wa hadhara mwenye uwanja fatma,katibu mkuu amemwagiza
mkuu wa mkoa huo Bwana John Mongela kusimamia tatizao la uvushwaji wa zao la
kahawa kwenda nchi jirani ya uganda,kwa kuwawekea bei nzuri ya soko,sanjali na
udhibiti vizuizi vya barabarani kwa zao la ndizi,na kusema kuwa hiyo ni kero
inayowakera wananchi wa muleba.
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida wananchi hao hasa wa visiwani wilayani muleba,walimweleza katibu
mkuu kitendo cha uongozi wa wilaya kutoa
siku mbili kwa uandikishaji wa daftari la wapiga kura,hatua ilimlazimu kaktibu
mkuu kusema kuwa hakuna sheria ya kupunguza siku za uandikishaji kwa kila eneo
lililotangazwa kuanza zoezi hilo nakudai kuwa kila eneo ni siku saba kwa nchi
nzima.
0 comments:
Post a Comment