Image
Image

Viongozi wa kundi la mataifa yaliyostawi zaidi kiviwanda G7, yamekata kauli kudumisha vikwazo.


Viongozi wa kundi la mataifa yaliyostawi zaidi kiviwanda G7, yamekata kauli kudumisha vikwazo walivyoiwekea Urusi hadi pale taifa hilo litakapotekeleza kikamilifu mkataba wa amani walioafikiana na Ukraine.
Uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha kila mwaka cha mataifa hayo tajiri.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amekariri kuwa vikwazo hivyo vimewekwa mahsusi ili kutatua tatizo hilo , na iwapo utawala wa Moscow utauendeleza mkataba huo wa amani basi bila shaka vitaondolewa.
Kwa mara ya pili tangu mzozo huo na Ukrain utokee rais Putin hakualikwa kwenye kikao hicho licha ya Urusi kuwa mwanachama wa G7.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment